WAINGEREZA WAWILI WAFUNGWA KWA UGAIDI ETHIOPIA

Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn.

Raia wawili wa Uingereza na msomali mmoja wamefungwa jela nchini Ethiopia kwa kupanga njama ya kuunda dola ya kiislamu.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa kituo cha redio kinachounga mkono serikali.
Taarifa hii imethibitishwa na ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza.
Wanaume hao watatu waliohukumiwa kifungo cha kati ya miaka minne na saba walidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la wapiganaji wa kiislamu.
Ethiopia ina sheria kali sana za kupambana na ugaidi.
Kwa muda mrefu imekuwa ikiendesha harakati dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Al shabaab nchini Somalia.
Nchi hiyo pia imekuwa ikikabiliwa na madai ya kuwafunga jela wakosoaji wa serikali wakiwemo wanablogu maarufu nchini humo ambao wanakabiliwa na tishio la kufungwa jela kwa madai ya kuhusika na ugaidi na wamekuwa wakizuiliwa tangu Aprili mwaka 2014.
Hata hivyo kiongozi wa nchi hiyo ametetea sana sheria kali za ugaidi ambazo nchi hiyo hutumia.
Kulingana na FBC, washukiwa wawili waingereza, Ali Adros Mohammad na Mohammad Sharif Ahmed walikuwa wanaishi mjini London wakati Mohammad Ahmed akiwa na mizizi yake Hargeisa eneo la Somaliland.
Watuhumiwa hao watatu inaarifiwa walikuwa na mawasiliano na wanachama wa kundi la wapiganaji wa kiislamu tangu mwezi Disemba mwaka 2012 na walisafiri kwenda mjini Adama, ambako walikuwa wanapanga kufanya mashambulizi ya kigaidi.
Mahakama kuu mjini Addis Ababa, iliarifiwa kuwa Ali Adros aliingia nchini Ethiopia kutoka Kenya kwa mafunzo ya kijeshi na kwamba pia alikuwa na makubaliano na kundi la waasi la (OLF), kufanya mashambulizi nao.





Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment