MWANAUME NI TORRES ASEMA DIEGO SIMEONE

Fernando Torres


Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone amesema Fernando Torres amerejea kuwa ''mwanaume'' ndivyo alivyomuita hivyo baada ya mshambuliaji huyo kufunga magoli yake ya kwanza tangu alipojiunga na Atletico madrid.

Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Torres alijiunga na Liverpool mwaka 2007.
Torres alijiunga na Atletico mwanzoni mwa mwezi huu na aliifungia klabu hiyo magoli mawili katika dimba la Bernabeu na kutoka sare ya mabao 2-2 ilipokutana na Real Madrid katika michuano ya Copa del rey
Torres naye ameonesha furaha yake na kushukuru wapenzi wake kwa kumuunga mkono kwa wakati wote.
Torres alipokelewa na mashabiki wengi katika utambulisho wake alipokuwa akirudi katika timu yake hiyo ya zamani na ilionyesha jinsi gani mashabiki wa Atletico wana imani na mshabuliaji huyo kihispania.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment