TETESI ZA USAJILI; DE GEA KUONDOKA MAN U

 Mlinda mlango namba moja wa Manchester United David De Gea.


Mustakabali wa kipa David de Gea kusalia Manchester United upo shakani baada ya wakala wake Jorge Mendes kushindwa kuwakatalia Real Madrid mpango wa kumsajili.

Manchester United inajianda kutoa ofa kwa timu ya Villarreal ili kumpata kumpata beki Gabriel Paulista, raia wa Brazil ambaye yuko kwenye mazungumzo na Arsenal.
Klabu ya Chelsea iko katika mipango ya kumsajili kiungo wa Shakhtar Donetsk Douglas Costa.
Bosi wa West Brom Tony Pulis amethibitisha kuhitaji kuwasajili winga wa Wigan Callum McManaman na kiungo Darren Fletcher toka Man United katika dirisha hili la usajili.
Timu ya QPR imetoa ofa ya kumsajili mshambuliji wa zamani Ac Milan Alexandre Pato,anayechezea timu ya Sao paul kwa mkopo.
Meneja wa Swansea City Garry Monk anavutiwa na mpango wa kumsajili beki wa kushoto wa Norwich Martin Olsson, mwenye umri miaka 26,pamoja na kiungo Alexandru Maxim toka Stuttgart.
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers anatarajia winga wake Raheem Sterling, atasaini mkataba wa muda mrefu kusalia klabuni hapo siku chache zijazo.
Manchester City wameulizia uwezekano wa kumpata mshambuliaji Jay Rodriguez wa timu ya Southampton.
Hull City wanamfuatilia winga wa Tottenham na timu ya Taifa ya England Aaron Lennon,ambae anataka kuondoka White Hart Lane kwa kukosa namba katika kikosi cha kwanza.
Kiungo wa zamani wa Chelsea Kevin de Bruyne,amekataa kurejea katika ligi ya England kwa kusema havutiwi kurudi katika ligi pamoja na kuwepo taarifa za kuwaniwa na Arsenal na Manchester United.
Klabu ya Roma inajaribu kuwashawishi Chelsea kukubali pauni 380,000 ili kumchukua winga Mohamed Salah kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment