Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ambacho kimefanyiwa maboresho
Timu ya Tanzania, Taifa Stars leo inakabiliana na majirani zao Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa katika jiji la Mwanza magharibi mwa Tanzania.

Akizungumza mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania, TFF, Boniface Wambura amesema maandalizi ya mchezo kati ya timu mbili hizo yanaendelea vizuri ikiwa pia ni fursa kwa timu hizo kujiandaa na mashindano yajayo ya Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, yanayowashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya nchi zao maarufu kama CHAN.
Rwanda ndiye mwenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka 2016.
Timu ya Rwanda pia imo katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza michezo ya Olympiki ya Rio De Janeiro nchini Brazil mwaka 2016.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment