Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, January Makamba |
Siku chache baada ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuonyesha kuwa CCM, imeporomoka, Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, January Makamba..
amewataka wanachama wa chama hicho kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote yanayoweza kutokea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
“Wana-CCM wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani
walizoea ushindi wa asilimia 90 au 80 (wa kishindo), huu ulikuwa ushindi
wa nyuma. Tusishangae tukipata ushindi wa asilimia 50, 60, 57 au 70 ni
kitu cha kawaida kutokana na kukua kwa demokrasia hususani ushindani wa
vyama vingi vya siasa kuanza kuimarika.
Kauli hiyo ya Makamba imekuja wakati matokeo ya
serikali za mitaa yakionyesha kuwa CCM imeporomoka kutoka ushindi wa
asilimia 91.7 mwaka 2009 hadi 79.8 katika uchaguzi wa mwaka jana na
upinzani ukipanda kutoka asilimia nane mwaka 2009 hadi takriban 20 mwaka
jana.
“Hata ushindi wa asilimia 81 tulioupata katika
uchaguzi wa Serikali za Mitaa bado ni mkubwa na hata kama tungepata
asilimia 70 haupunguzi uhalali wa uongozi. Kusema CCM itang’oka
madarakani, hapana, bado wananchi wanakiamini tena sana,” alisema
Makamba.
Makamba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, alizungumzia pia namna ya kuwapata wagombea wa urais na
kusema mwaka huu ndiyo utapima ukomavu wa chama katika harakati za
kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete.
Makamba ambaye Julai 2, mwaka jana akiwa
London, Uingereza alitangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, alisema
mwaka 1995 mgombea alipatikana kwa malezi ya Mwalimu Julius Nyerere,
mwaka 2000 aliendelea aliyekuwapo.po. Alisema mwaka 2005 ilikuwa kama
1995 lakini mwaka huu ni tofauti na vipindi vingine kabisa.
“Hii ni mara ya kwanza hakuna uhakika wa nini
kitatokea na kwa mara ya kwanza chama chetu kama taasisi kitajaribiwa...
na sisi tuna utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa.
“Tuna sifa 13 za kumpata mgombea, sifa hizi na
taratibu nyingine zikifuatwa tutampata. Mchakato ukiwa wa haki tutampata
kwani nina imani na mwenyekiti (Rais Kikwete), Katibu Mkuu (Abdulrahman
Kinana) na Kamati Kuu,” alisema Makamba .
Ujana na uzee
Kuhusu hoja ya ujana au uzee ambayo imewagawa
wagombea urais wa CCM, Makamba alisema kuna tofauti kati ya umri, uwezo
na uzoefu ili wananchi waweze kumwamini mtu na kumpa fursa ya
kuwatumikia, jambo ambalo alisema halihitaji kutumia fedha nyingi au
kuweka mbele uchu wa madaraka ili kuyafanya mazingira yawe ya lazima
kupata.
Credit; Mwananchi
Credit; Mwananchi
0 comments :
Post a Comment