CHADEMA KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU

Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dk. Wilbroad Slaa (kushoto) akiwa na Mwanasheria Tindu Lissu

Wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ikisisitiza kuwa ratiba ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura itaenda kama ilivyopangwa, kamati kuu ya chama cha Demokrasi na Maendeleo imesema itachukua maamuzi magumu endapo shughuli za uboreshaji huo zitachelewa na kuharibu mchakato wa kura ya maoni.

Mkurugenzi wa NEC, Julius Malaba alisema leo kuwa uboreshaji utaanza Februari 16 kama ilivyotangazwa awali na utamalizika kwa wakati ili kupisha ratiba ya kura ya maoni.
“Ratiba inazingatiwa, vifaa vitafika kwa wakati na kuanza kazi kwa wakati,” alisema Malaba.
Akizungumza wakati wa kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya Chadema, Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema chama hicho kimeitisha kikao hicho ili kujadili hatma ya uboreshaji wa daftari hilo na muda uliobaki kabla ya kupiga kura ya maoni Aprili 30, mwaka huu.
Pia Chadema walisema kuwa watachukua hatua zaidi iwapo mashine za Biometric Voters Registration(BVR) zitabainika kuwa na kasoro katika uboreshaji huo.
Zoezi la kuandikisha Watanzania milioni 26 wenye sifa ya kupiga kura lilitakiwa kuanza mwezi huu lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema zoezi hilo litaanza Februari 16, mwaka huu kwa sababu bado inasubiri mashine 7,750 za (BVR) kwa ajili ya kazi hiyo.
 “Kwa mazingira ya kawaida muda uliobaki kwa ajili ya kazi hiyo kubwa hautoshi ndiyo maana kuitishwa kwa kikao cha dharura ili kufanya uamuzi,”alisema Makene.




Credit; Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment