Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema. |
WATU 15 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za kivita na mabomu ya kurushwa kwa mkono wamevamia kituo cha polisi Ikwiriri wilayani Rufiji Mkoani Pwani na kuua askari polisi wawili na kupora silaha tano za SMG na mbili za kufyatulia mabomu ya machozi zilizokuwepo kituoni hapo na kutokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Ulrich Matei
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa majambazi hao
wamefanikiwa kuchukua silaha tano za moto na mbili za mabomu ya machozi
zilizokuwepo kituoni hapo.
Amesema polisi wawili Koplo Edga na WP Judith
wamethibitika kuuawa na majambazi hao katika tukio hilo na kwamba
jitihada zinaendelea kuwatafuta waliohusika na tukio hilo.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zimesema kuwa
majambazi hao walivamia kituo hicho saa mbili usiku na kuwakuta maofisa
hao wa polisi wakiwa katika zamu ya usiku bila kuwaeleza chochote
wakaanza kuwashambulia kwa risasi.
Majina ya polisi waliouawa yametajwa kuwa ni koplo Edgar na askari wa kike Judith ambao walipigwa risasi .
Mmoja wa wakazi wa mji wa Ikwiriri Arafa Ngwaya
amesema usiku wa kuamkia jana kulisikika milio kadhaa ya risasi na
milipuko ya mabomu lengo likiwa ni kutisha wananchi na polisi kutotoka
nje kutoa msaada wakati wa utekelezaji wa shambulio hilo.
“Tumepatwa na taharuki kubwa katika tukio hili na
inaonekana hawa jamaa walijizatiti vilivyo, Polisi kwa kutumia vitengo
vyetu mahususi vya upelelezi tunaendelea kufanya uchunguzi, pia
tunawaomba raia wema ambao wana taarifa zozote za majambazi hao
watufahamishe”alisema Kamanda Matei.
Credit; Mwananchi
Credit; Mwananchi
0 comments :
Post a Comment