MSICHANA WA MIAKA KUMI AJILIPUA


Eneo la soko ambapo mlipuko huo umetokea kaskazini mashariki katika mji wa Maiduguri.
Mlipuaji wa kujitolea muhanga amejilipua katika soko moja katika mji wa kazkazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.

Baadhi ya ripoti zinasema kuwa mlipuaji huyo ni msichana wa miaka kumi.
Duru kutoka hospitali zimesema kuwa takriban watu 15 wameuawa.
Hakuna mtu aliyekiri kutekeleza shambulizi hilo kufikia sasa.
Hatahivyo watu wanalishuku kundi la Boko Haram kutokana na misururu yake ya mashambulizi katika mji huo na maeneo mengine ya Nigeria Kaskazini.
Takriban watu elfu ishirini wamelazimika kutoroka na inahofiwa kuwa mamia waliuawa wakati Boko Haram lilipochukua udhibiti wa mji wa Baga na viungani mwake wiki iliopita.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment