AKAMATWA AKITOROSHA KENGE NJE YA NCHI

Uwanja wa ndege wa  kimataifa wa Julius Nyerere International Airport(JNIA) Dar es salaam.

Jeshi la Polisi la   Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)linamshikilia raia wa Kuwait kwa tuhuma za kukutwa na viumbe hai aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.

Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Hussain Ahmed Ally Mansour(34), raia wa Kuwait ambaye alikamatwa uwanjani hapo jana  majira ya saa 5 usiku wakati akijiandaa  na safari ya  kuelekea nchini Kuwait  kupitia Dubai  na Shirika la Ndege la Emirates  .
Kamanda  Selemani amesema Mansour alikamatwa na wanyama hao ambao aliwahifadhi  kwenye mifuko midogo midogo ilivyowekwa katika begi kubwa lenye rangi nyeusi.
“Kenge waliwekwa kwenye mifuko midogo midogo 15 na kila mmoja una kenge 15 na mifuko mingine walikaa wawili,”alisema kamanda Selemani.
Alisema kati ya Kenge hao, 15 walikufa na walio hai walikuwa 134 ambao  walikuwa wamefichwa kwenye mifuko hiyo.
 
Seleman alisema wakati wanafanyiwa upekuzi ndipo  walipogundua kuna vitu ambavyo vinafanana na nyoka  na kuamua  kuwashirikisha wataalamu wa maliasili ambao walibaini kuwa begi hilo lilikuwa na Kenge.
“Huyu mtuhumiwa alikuja nchini Januari 6,alitiliwa mashaka na polisi wa JNIA  na tulimuamuru akae pembeni kwa upekuzi zaidi  na kugundua anasafirisha kenge bila Kibali,”alisema Selemani.
Selemani alisema walipoendelea kumuhoji mtuhumiwa huyo alidai kuwa alikuja nchini kwa ajili ya kuchukua viumbe aina ya ndege lakini baada ya kuwakosa aliamua kubeba Kenge hao.
Kamanda Selemani aliwaomba wananchi kuwa na uzalendo wa nchi yao wanapoona mtu anasafirisha rasilimali za nchi watoe taarifa katika jeshi la polisi.




Credit; Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment