CHELSEA KUMNYAKUA MESSI KWA PAUNI MILIONI 200

Mshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Barcelona na nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi.

 Lionel Messi ameambiwa kwamba kuna mkataba wa miaka sita kutoka kwa kilabu ya Chelsea unaomngojea.

Duru za karibu na mchezaji huyo wa Barcelona zinaarifu kuwa Chelsea imeweka wazi kwamba iko tayari kutoa kitita cha pauni millioni 200 kumnunua nyota huyo.
Vilevile The Blues imedaiwa kwamba iko tayari kulipa mahitaji yake ya mshahara ambayo huenda yakaongeza kiwango hicho mara mbili.
 
Mnamo mwezi Novemba kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikana habari zinazoihusisha kilabu hiyo na Messi,lakini katika kilabu ya Barcelona kumekuwa na mgogoro tangu wakati huo na ripoti kutoka Uhispania zinasema kuwa mchezaji huyo amekuwa akizozana na muajiri wake Luis Enrique.
Inadaiwa kuwa Messi hakushiriki katika mazoezi ya siku ya jumatatu huku Enrique akishindwa kukana mgogoro uliopo kati yake na Messi.



Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment