MAGARI YENYE PICHA ZA RAISI KUKAMATWA



Licha ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuruhusu magari yanayobeba abiria nchini Kenya kuchorwa ama hata kupaka rangi yoyote ile
,mabasi mawili yaliyoochorwa picha yake yamekamatwa na maafisa wa polisi mjini Mombasa Kenya.
Maafisa wa trafiki mjini Mombasa waliyakagua magari hayo na kuyakamata magari yote yaliyokuwa yamechorwa picha pamoja na magari yenye madirisha yasiyoonyesha ndani.
Magari sita yakiwemo mawili yaliyokuwa na picha ya Uhuru yalikamatwa,licha ya agizo la rais kuruhusu wamiliki wa matatu kuchora picha katika magari.
Uhuru alikuwa amesema kuwa hatua hiyo itawasaidia vijana kutumia vipaji vyao ili kuweza kujinufaisha kimaisha.
Uchoraji katika magari hayo na muziki ulipigwa marufuku mnamo mwaka 2003 na aliyekuwa waziri wa uchukuzi John Michuki.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment