Mamia ya wanajeshi wanashika zamu
mjini Paris baada ya siku tatu za ugaidi zilizouwa watu 17, huku taarifa
zikitokeza kuhusu jinsi mfanyakazi Muislamu wa
supermarket ya Wayahudi
mjini Paris alivyowaficha wateja 15 pamoja na mtoto mchanga wa mwezi
mmoja wakati duka hilo liliposhambuliwa na gaidi.Aliwaficha wateja kwenye chumba cha barafu.
Lassana Bathily, kijana wa asili ya Mali, aliiambia televisheni ya Ufaransa kuwa aliwaongoza wateja waliokuwa wamebabaika, hadi chumba cha chini kwa chini.
Alizima mtambo wa barafu na kuwaomba wakae kimya na alirudi juu dukani.
Askari wa usalama wakiweka doria katika eneo lililofanyiwa uvamizi huko Paris. |
Baada ya duka hilo kukombolewa na askari wa usalama, Lassana Bathily alisema wateja walimshukuru kwa kunusuru maisha yao.
Credit; BBC
0 comments :
Post a Comment