Watu wakiwa katika mitaa mbalimbali nchini Dubai.

Dubai imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za jamii kwa pochi iliyoangushwa mtaani,na ikarejeshwa kwa mhusika mara moja.

Katika utafiti uliofanywa na mtengeneza Filamu mwenye asili ya Uingereza katika mitaa ya Dubai, alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha kwa makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi hiyo kwa mmiliki wake.
Daniel Jarvis, mwenye miaka 26,akiwa ameificha kamera yake na kurekodi mfululizo wa matukio hayo ya makusudi akiwa pamoja na rafikiye aliyejipachika jina la utani la 'Digi' ama Dan, mwenye miaka 25, walibarizi katika viunga vya Downtown na Bur vilivyoko Dubai,siku za karibuni na kuweka swali je unaweza kuiba Dubai? Kutaka kuichunguza jamii na kurushwa vipande vyake katika YouTube ambapo kwa siku kadhaa watazamaji walikuwa ni zaidi ya 70,000 .
Jarvis aliiambia 7DAYS walishangazwa na utafiti huo na kikubwa kilichowashangaza ni kwamba walio okota pochi hiyo hawakujishughulisha kutazama ndani kuna nini? Wakati pochi hiyo ilikuwa imesheheni euro za kutosha na fedha ya Falme za Kiarab dirham kadhaa.
Mtaa wa kwanza walioufanyia majaribio ni mtaa ulio katika barabara ya Sheikh Zayed karibu na soko kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara wa Emirates lakini kila aliyeiona pochi hiyo aliirejesha,lakini baadaye tukafikiri sababu ya kurejeshwa pochi hiyo kuwa walioko eneo hilo ni matajiri.
Basi utafiti wetu tukauhamishia eneo la Bur ,Dubai, mahali ambapo palionekana duni kidogo cha ajabu watu waliendeleza utamaduni ule ule wa kurejesha pochi kama ilivyo, na hali iliendelea hivyo mara kadhaa.
Jarvis anasema wameshafanya utafiti kama huo katika mji wa London nchini Uingereza. Na huko walistaajabu walipoidondosha tu aliyeiokota alianza kukimbia nayo na hakuna aliyethubutu kuirejesha pochi hiyo.
Jarvis, alivalia suti nadhifu na kuigiza kudondosha pochi anaonekana kwenye video hiyo anaeleza hisia za kurejeshewa kitu ulichondondosha kuwa ni raha iliyoje .lakini akaendelea kusema kuwa anadhani vyombo vya habari hupotosha ukweli,kwakuwa kulikuwa na kichwa cha habari kuwa kuna mtu alihukumiwa miaka 15 jela kwa kuiba mdoli wenye taswira ya dubu, utafiti wetu umegundua tofauti na wayasemayo.
Trollstation ina wanachama wapatao 230,000 na utafiti wao kutoka Falme za Kiarab unaelekezwa Ulaya, Marekani na hatimaye Afrika .
Inawezekana katika maeneo watakayopita kuvunja rekodi ya Dubai tusubiri wakati uwadie, ni kauli yake Jarvis .




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment