HATMA YA YAYA TOURE MANCHESTER CITY

Yaya Toure kiungo mshambuliaji wa Manchester City na Timu ya taifa ya Ivory Coast.

Mchezaji nyota katika klabu ya Manchester City Yaya Toure amesema kuwa hajui hatma yake ya kuichezea klabu hiyo msimu ujao.
Lakini Meneja Manuel Pelegrini alikuwa wa haraka kufutulia mbali madai ya uhamisho wake akisisitiza kuwa mchezaji huyo wa kiungo cha kati nia yake ni kusalia katika klabu hiyo.
Yaya Toure ambaye ambaye ametajwa kama mchezaji bora wa bara la Afrika mwaka huu alijiunga na ligi ya Uingereza mnamo mwaka 2010 kutoka Barcelona na amepata mafanikio si haba katika uwanja wa Etihad Stadium.
 
Lakini katika kipindi cha mwaka uliopita,uhusiano kati ya klabu hiyo na Yaya si mzuri huku mchezaji huyo akidai kutofurahishwa na hatua ya klabu hiyo kusahau siku yake ya kuzaliwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment