ARSENAL YAICHARAZA MANCHESTER CITY ETIHAD

Kiungo mshambuliaji wa Arsenal  Santi Carzola akipiga mkwaju wa penati na kuipatia timu yake goli dhidi ya Manchester City

Santi Carzola alifunga bao moja na kutengeza jengine na kuisadia Arsenal kuicharaza Mancity mabao 2-0 nyumbani Manchester.

Ushindi huo wa Arsenal pia ulisitisha msururu wa kutofungwa wa Mancity wa mechi 12.
Mchezaji wa Uhispania Santi Carzola aliyekuwa moto wa kuotea mbali dhidi ya Mancity alifunga kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Arsenal Nacho Monreal kuangushwa katika eneo la hatari na beki Vincent Kompany.
Wachezaji wa Arsenal Olivier Giroud kulia akimpongeza mchezaji mwenzake Santi Carzola baada ya wote wawili kufunga katika mechi dhidi ya Manchester City.

Arsenal iliongeza bao la pili katika kipindi cha pili baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Santi Carzola kuwekwa wavuni na Olivier Giroud.
Matokeo hayo yameiacha City ikiwa na alama 5 chini ya viongozi wa ligi Chelsea.
City na Arsenal walitoka sare ya 2-2 wakati walipokutana kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Emirates mnamo mwezi Septemba.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment