Daktari akimpa matibabu muathirika wa ugonjwa wa Ebola katika moja vituo vya kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola. |
Serikali ya Sierra Leone imetangaza
siku tatu za marufuku ya kutotoka nje kaskazini mwa taifa hilo, ili
kuruhusu jitihada za kukabiliana na kuenea zaidi kwa ugonjwa hatari wa
Ebola.
Msemaji wa serikali amesema kuwa maduka na masoko yatafungwa na hakuna magari ya abiria au pikipiki yatakubaliwa kwenye barabara za eneo hilo.
Sherehe za makanisa kuadhimisha sherehe za siku ya Krismasi pia zimepigwa marufuku katika ukanda huo.
Sierra Leone ni mojawapo ya mataifa ya Afrika magharibi ambayo yalikumbwa kwa sehemu kubwa na ugonjwa huo wa ebola ambao pia umeleta maafa makubwa mpaka sasa.
0 comments :
Post a Comment