mwaka huu umetajwa kuwa ni mwanzo wa mwisho wa Ukimwi, lakini wanaharakati wanasema bado hiyo haimaanishi kwamba maradhi haya thakili yatamalizika hivi karibuni.

Kenya, taifa la nne duniani kwa kuwa na maambukizi mengi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) imeshuhudia kiwango kikubwa cha kupungua kwa maambukizi mapya ndani ya kipindi cha miaka ya hivi karibuni, ingawa hali kwenye mitaa ya mabanda katika mji mkuu Nairobi ni ngumu, hasa kwa wanawake ambao bado wanaishi chini ya kivuli cha ugonjwa huo.
Takribani theluthi moja ya wakaazi wa Nairobi wanaishi kwenye mtaa wa madongo-poromoka wa Kibera, ambako mtu mmoja katika kila watano anaishi na VVU. Kwenye mtaa huu, wanawake wengi masikini hulazimika kujiingiza kwenye biashara ya ngono ili kujikimu kimaisha, wakiwa hawana muamko wa kujikinga.
"Ukosefu wa pesa ni sababu kubwa kwa wanawake wa Kibera kuambukizwa VVU. Wanawake hawana pesa ya kuwawezesha kuishi, hivyo wanawageukia wanaume kuomba msaada, ambao nao kawaida hudai penzi na wanakataa kuvaa mipira ya kiume, na hivyo ndivyo hupata pesa kwa ajili ya chakula na watoto wetu, lazima tukubali na hivyo tunaambukizwa," anasema Caroline Akoth, mjane anayeishi kwenye mtaa huu wa mabanda na ambaye kazi yake ya udobi na kuuza vinywaji inaweza kumpatia dola mbili tu kwa siku.
Msaada wa matibabu
Caroline alianza kupata matibabu miaka mitano iliyopita kwa msaada wa jumuiya moja isiyo ya kiserikali. Miongoni mwa wafanyakazi wa huduma za kijamii kwenye mtaa wa Kibera ni Joyce Waithera Wambui, ambaye anasema huwasaidia wanawake wote wanaoshi kwenye mazingira magumu.
"Wanawake hawa wanahitaji msaada zaidi. Tunawafunza stadi za maisha, hatua za kujikinga na afya kwa ujumla. Kwa wale amba tayari wameshaambukizwa, tunawagawia mipira ya kinga na kuwaambia namba ya kuishi na kuvidhibiti virusi hivyo."
Kufikia mwaka jana, asilimia sita ya wale wanaoishi na VVU nchini Kenya walikuwa na umri wa kati ya miaka 15 na 49. Mwaka 1996, hali ilikuwa mbaya zaidi, ambapo asilimia 10.8 walikuwa wameambukizwa .
kuwa hadi kufikia mwaka jana, watu milioni 35 duniani walikuwa wanaishi na ugonjwa huo, huku milioni 2.1 wakiwa wagonjwa wapya na milioni 1.5 wakifariki dunia kutoka




Credit; DW
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment