Bondia Floyd Mayweather wa Marekani akionyesha mwili wake kabla ya pambano lake |
Kama unavyojua michezo ni afya kwa kuwa inajenga na kuimarisha miili yetu inakua imara lakini pia michezo ni ajira kama zilivyo ajira nyingine ukiachilia mbali suala la kufurahisha watu kwa ujumla lakini vilevile wanapata fedha nyingi kutokana na matangazo ya kibiashara, tuzo za fedha na ujira.
Wafuatao ni wanamichezo 20 waliolipwa fedha nyingi zaidi mwaka 2014 kwa mujibu wa Jarida la Forbes la Marekani:
20. Kevin Durant, Marekani (Kikapu)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 31.9 milioni.
Nyota huyu wa kikapu anayechezea timu ya Oklahoma
City Thunder ya Marekani alishinda tuzo ya mchezaji mwenye thamani ya
juu katika Ligi Kuu ya kikapu nchini Marekani (NBA), pia aliiwezesha
Thunder kushika nafasi ya pili mwaka huu. Mchezaji huyu ametwaa tuzo ya
mfungaji bora NBA mara nne.
19. Lewis Hamilton, England (Mbio za magari)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 32 milioni.
Alijiunga na timu ya Mercedes F1 mwaka 2013 ili
apate udhamini mkubwa. Nyota huyu wa mashindano ya magari ya F1 anatajwa
kuwa kati ya madereva bora zaidi katika mchezo huo.
18. Matthew Stafford, Marekani (American Football)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 33 milioni.
Mwezi Julai 2013, Stafford aliongeza mkataba na
kusaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea timu ya Detroit Lions ya
mchezo wa American football, mkataba ambao ulikuwa na thamani ya Dola za
Marekani 53 milioni, pia alipewa fedha za ziada za kusaini mkataba dola
27.5 milioni. Hata hivyo fedha alizopata mwaka huu kutokana na
matangazo ya kibiashara, tuzo na ujira ni dola za Marekani 33 milioni.
17. Novak Djokovic, Serbia (Tenisi)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 33.1 milioni.
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 33.1 milioni.
Bingwa huyu mtetezi wa taji la Wimbledon alitwaa
mataji mengine matano makubwa mwaka huu katika mchezo wa tenisi na hivyo
kuingiza zaidi ya Dola za Marekani 9 milioni zikiwa ni tuzo za fedha.
Pia alipata mikataba ya matangazo ya biashara na Peugot na Seiko mwaka
huu.
16. Neymar, Brazil (Soka)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 33.6 milioni.
Mwaka 2013, Neymar alijiunga na klabu ya Barcelona
kwa mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya dola za Marekani 74
milioni. Mwaka huu alipata mikataba mikubwa ya matangazo ya biashara na
Castrol, Police sunglasses na L’Oreal.
15. Radamel Falcao, Colombia (Soka)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 35.4 milioni.
Mwaka 2013, Falcao alisaini mkataba wa miaka
mitano wa kuichezea AS Monaco ya Ufaransa baada ya kupata mafanikio
makubwa katika klabu ya Atletico Madrid. Mwaka huu Falcao alijiunga na
klabu ya Manchester United ya Englandn kwa mkopo.
14. Gareth Bale, England (Soka)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 36.4 milioni.
Mwaka 2013, Real Madrid ilitumia kiasi cha dola za
Marekani 118 kumsajili Bale. Akiwa katika klabu hiyo, Bale amenufaika
sana na fedha za matangazo ya biashara, tuzo za fedha na ujira.
13. Derrick Rose, Marekani (Kikapu)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 36.6 milioni.
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 36.6 milioni.
Mwaka 2011, Derrick Rose alisaini mkataba wa miaka
mitano wa kuichezea timu ya kikapu ya Chicago Bulls ya Marekani.
Mkataba huo ulikuwa na thamani ya dola za Marekani 95 milioni. Hata
hivyo kutokana na kuwa majeruhi ameshindwa kuonyesha kipaji chake kwa
kiwango cha juu. Hata hivyo mwaka huu ameendelea kunufaika na matangazo
ya kibiashara na ujira.
12. Zlatan Ibrahimovic, Sweden (Soka)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 40.4 milioni.
Mwaka 2013 aliongeza mkataba wake wa kuichezea
Paris Saint-Germain mpaka 2016. Ibrahimovic anaingiza fedha nyingi kwa
matangazo ya biashara na Kampuni ya Volvo.
11. Manny Pacquiao, Philippines (Ngumi)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 41.8 milioni.
Bondia Pacquiao aliingiza fedha nyingi mwaka huu baada ya kuwachapa mabondia Brandon Rios na Timothy Bradley.
10. Matt Ryan, Marekani (American Football)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 43.8 milioni.
Mwaka 2013, Ryan anayecheza American Football
alisaini mkataba wa miaka mitano na Falcons wenye thamani ya Dola za
Marekani 103.75 milioni. Pia alilipwa dola za Marekani 28 milioni zikiwa
ni fedha za kusaini mkataba. Mwaka huu amenufaika zaidi na fedha za
matangazo ya kibiashara na ujira.
9. Rafael Nadal, Hispania(Tenisi)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 44.5 milioni.
Bingwa huyu wa mataji makubwa ya tenisi (French
Open, US Open) wa mwaka 2013, katika mwaka huu alipata Dola za Marekani
14.5 milioni zikiwa ni tuzo za fedha, pia yupo katika nafasi za juu
katika viwango vya wachezaji tenisi duniani hivyo kunufaika zaidi na
fedha za ziada kutoka kwa wadhamini.
8. Phil Mickelson, Marekani (Gofu)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 53.2 milioni.
Alipata fedha nyingi za ziada kutoka kwa wadhamini
mwaka jana baada ya kushinda taji la British Open katika mchezo wa gofu
hivyo mwaka huu kupata matangazo ya kibiashara ambayo yalimuingizia
zaidi ya Dola za Marekani 40 milioni.
7. Roger Federer, Uswisi (Tenisi)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 56.2 milioni.
Federer anashikilia rekodi ya kutwaa mataji
makubwa ya mchezo wa tenisi kwani ametwaa mataji 17 na tuzo za fedha
Dola za Marekani 81 milioni. Mwaka huu, Federer amenufaika zaidi na
matangazo ya biashara.
6. Tiger Woods, Marekani (Gofu)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 61.2 milioni.
Mcheza gofu Tiger Woods angeweza kupata fedha
nyingi zaidi, lakini kashfa za uhusiano na mpenzi wake alizozipata mwaka
2013 zilisababisha akose matangazo muhimu ya biashara
5. Kobe Bryant, Marekani (Kikapu)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 61.5 milioni.
Bryant analipwa mshahara wa dola za Marekani 30.5
milioni kikiwa ni kiwango kikubwa kwa wachezaji wote wa mchezo wa
kikapu, pia mwaka huu alipata matangazo ya biashara yanayokadiriwa
kufikia dola za Marekani 30 milioni.
4. Lionel Messi, Argentina(Soka)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 64.7 milioni.
Kampuni ya Adidas na Shirika la ndege la Uturuki
zimewekeza fedha nyingi kwa nyota huyu wa soka. Mwaka huu Messi amepata
fedha nyingi kutokana na fedha za matangazo na ujira. Pia anauza viatu
vingi vyenye saini yake.
3. LeBron James, Marekani (Kikapu)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 72.3 milioni.
LeBron ni mchezaji ambaye anapata fedha nyingi za
matangazo ya biashara katika Ligi Kuu ya kikapu nchini Marekani (NBA).
Makampuni yanayomtumia katika matangazo ni Nike, Coca Cola na
McDonald’s. Pia anaingiza fedha nyingi kwa kuuza viatu vyenye saini
yake.
2. Cristiano Ronaldo, Ureno(Soka)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 80 milioni.
Mwaka 2013, Ronaldo alichaguliwa kuwa mchezaji
bora wa dunia na tayari ameongeza mkataba wa miaka mitano wa kuendelea
kuitumikia klabu hiyo, mkataba huo una thamani ya dola za Marekani 206
milioni. Ronaldo alipata fedha nyingi mwaka huu kutokana na matangazo ya
kibiashara, tuzo za fedha na ujira.
1. Floyd Mayweather, Marekani (Ngumi)
Kwa ujumla alipata: Dola za Marekani 105 milioni.
Ni mwanamichezo ambaye ameingiza zaidi ya dola za
Marekani 100 milioni mwaka huu kwa mujibu wa jarida la Forbes. Mayweather
ndiye bondia na mwanamichezo anayelipwa fedha nyingi hivi sasa kabla hajapanda
ulingoni. Mbali ya fedha nyingi za matangazo ya biashara kwa mwaka huu,
pia alipata fedha nyingi kwa kupigana na Marcos Maidana.
0 comments :
Post a Comment