NDOA ZA UTOTONI ZAKITHIRI NCHINI TANZANIA

Katika ripoti hiyo Human Rights Watch inaelezea visa vya wasichana walioolewa wakiwa na umri mdogo kabisa, wengine hata miaka saba.

Shirika hilo linaitaka serikali ya Tanzania kuamuru umri wa mtu kuoa au kuolewa uwe miaka 18, likisema kwamba wasichana wanaoolewa wakiwa wadogo wananyimwa haki zao za msingi.
Ripoti ya Human Rights Watch yenye kurasa 75 inaelezea maisha ya wasichana walioolewa wakiwa wadogo. Brenda Akia ni mmoja wa watafiti walioandaa ripoti hii. "Baada ya kuolewa wanakutana na matumizi ya nguvu. Waume zao wanawapiga, wanawalazimisha kulala nao. Hawawapi hela za matumizi hivyo wasichana hao kiujumla hawana furaha."
Sheria zinaruhusu
Sheria ya ndoa ya mwaka 1971, inasema umri wa chini wa msichana kuolewa ni miaka 15 huku mvulana akitakiwa awe ametimiza miaka 18 kabla ya kuoa. hata hivyo, watoto wenye umri kuanzia miaka 14 wanaweza kuoana iwapo mahakama itatoa ruhusa.
Human Rights imeikosoa Tanzania kwa kushindwa kuweka sheria mpya kwenye rasimu ya katiba, sheria itakayomtaka mtu awe amefikisha miaka 18 kabla ya kuoa au kuolewa. Ingawa idadi ya watoto wanaofunga ndoa imepungua katika miaka iliyopita, idadi hiyo bado ni kubwa. Kwa mujibu wa takwimu za serikali, asilimia 40 ya wanawake waliolewa kabla ya kufikisha miaka 18.
Mfano mmoja ni msichana Anita. Baba yake alimlazimisha kuolewa alipokuwa na miaka 16. Wakati huo alikuwa akisoma kidato cha pili. "Baba yangu aliniambia kuwa hana hela ya kunilipia ada. Baadaye niligundua kuwa alikuwa ameshapokea mahari ya ng'ombe 20.



Credit; DW
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment