MAKAMU WA RAIS NA NJAMA YA KUMUUA RAIS

Makamu wa Rais nchini Zimbabwe, anasema anapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya shirika la habari la kitaifa kwa kumhusisha na njama ya kumuua Rais Robert Mugabe.

Joyce Mujuru amesema amewaamuru mawakili wake kumrejeshea hadhi yake ya kisiasa baada ya kuhusishwa na madai hayo ya uhaini pamoja na ufisadi.
Jarida la Sunday Mail la nchini humo, limeripoti kuwa kuna njama ya kumkodi mamluki kumuua Mugabe ili Bi Mujuru achukue mamlaka.
Mwezi jana Bwana Mugabe alifikisha miaka 90 na kusema hana nia ya kuachia madaraka.
Ametawala Zimbabwe tangu nchi hiyo kujipatia uhuru mwaka 1980.
'Ushetani'
Rais Mugabe na Bi Mujuru walikuwa wandani wa karibu lakini kwa sasa wamehasimiana huku mjadala wa kumrithi Mugabe ukitokota katika chama tawala cha Zanu-PF kikijiandaa kwa kongamano lake la kitaifa mwezi ujao.
Mkewe Bwana Mugabe, Grace Mugabe amekuwa akiendesha kampeni dhidi ya Bi Mujuru akimtaka astaafu.
Amemtuhumu Bi Mujuru kwa kuwa mtu wa kishetani na mwenye kugawanya watu pamoja na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu, kutoka kwa makampuni.
Taarifa ya bi Mujuru akikana madai ya njama hiyo haikutarajiwa.
Ingawa hajaonyesha dalili za kuachia ngazi, anakabiliwa na shinikizo kali sana za kisiasa.
Jarida la Sunday mail liliripoti taarifa hizo za kushtua kwamba bi Mujuru na washirika wake wanapanga kumkodi mamluki ambaye atamuua Mugabe ili achukue mamlaka.
"ninakanusha madai hayo ya uhaini na ufisadi pamoja na kutumia vibaya mamlaka yangu, madai ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi yangu kwa muda mrefu sasa,'' alisema Mujuru.
Amewataka mawakili wake kuchukua hatua za haraka za kisheria dhidi ya waliotoa madai hayo na kumharibia sifa yake.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment