MOMBASA NA MSAKO MKALI WA MISIKITI

Polisi nchini Kenya wanasema kuwa wamenasa maguruneti na silaha nyinginezo usiku wa kuamkia leo katika msako mkali walioanza kufanya dhidi ya misikiti inayodaiwa kutoa mafunzo ya itikadi kali za kidini mjini Mombasa pwani ya Kenya.
Mtu mmoja aliuawa na wengine zaidi ya 250 kukamatwa katika msako huo unaolenga misikiti inayosemekana kutoa mafunzo kuhusiana na harakati za wapiganaji wa kiisilamu wa Al Shabaab nchini Somalia.
Polisi wanadai kuwa misikiti hiyo ikiwemo Masjid Musa inatumika kwa kuwasajili vijana wanaojiunga na Al Shabaab nchini Somalia.
Msikiti mwingine uliolengwa ni ule wa Sakina.
Mkuu wa polisi mjini Mombasa alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa walipata taarifa kwamba kundi hilo limekuwa likipanga kufanya mashambulizi na hiyo ndio sababu ya msako huo kuanzishwa.
Watu 200 wamekamatwa ikiwemo washukiwa wakuu sita.
Polisi wanasema kuwa mtu mmoja aliuawa ingawa hawajatoa taarifa zaidi kuhusu kifo cha mtu huyo na kwamba uchunguzi utafanywa.
Viongozi kadhaa wa kidini wameuawa mjini Mombasa katika kinachodaiwa kuwa mauaji ya kiholela huku kukiwa na ushindani pamoja na uhasama kati ya makundi kinzani ya kiisilamu.
Makanisa pia yamekuwa yakilengwa kwa mashambulizi.




Credit;BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment