AJIKATA SEHEMU ZA SIRI AKITAKA KUBADILISHA JINSIA

Msanii Mrusi aliyecheza katika filamu mashuhuri ya 'Burnt by the Sun 2', alipoteza uume wake baada ya kujikata akitaka kuwa mwanamke.
Kikubwa kilichomfanya msanii huyo Evgniv Sapaev kujitaka sehemu zake za siri ni kwamba alitaka sana kuwa mwanamke.
Mwanamume huyo alionekana akitoka nje ya nyumba yake huku damu ikimwagika kutoka kwa sehemu zake nyeti kufuatia upasuaji aliojifanyia mwenyewe.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye nyota yake ilikuwa inang'ara sana alikimbizwa hospitalini kwa huduma ya dharura kwa hofu ya hali yake kuwa mbaya .
Madaktari walijaribu kumshona lakini hawakufanikiwa katika juhudi zao za kumrejeshea mwanamume huyo uume wake.
Afisa mmoja hospitalini ambako muigizaji huyo alipokea matibabu alisema alikuwa na bahati sana kupona kwani alivuja damu nyingi na kwamba angepoteza muda kidogo tu angefariki.
Kwa mujibu wa jarida la Mirror, jirani ya Evgniv Sapaev, Arkhip Tikhonov mwenye umri wa miaka 57 alishtuka sana alipombishia mlango na kujionea hali yake akiwa tayari ameanza kudhoofika kwani alikuwa amepoteza damu nyingi sana.
''Alionekana akitisha sana akiwa na damu mikononi mwake huku akishika sehemu yake ya uume ambayo alikuwa ameikata. Nilidhani alikuwa anafanya mazoezi ya uigizaji, lakini alipozirai mlangoni huku akiwa ameshika sehemu yake ya siri mkononi ndipo nilipogundua kuwa mambo yalikuwa mabaya,'' alisema jirani wa Evgniv
Baada ya kupata nafuu mwathiriwa alinukuliwa akisema, ''tangu niwe mtoto mdogo nimekuwa nikijihisi kuwa mwanamke. Nilijaribu mara nne kukata nyeti zangu lakini wakati wote sikuwa na ujasiri wa kufanya hivyo.Lakini wakati huu niliweza kufanya hivyo baada ya kumeza tembe za kuzuia maumivu, na kujitaka kwa kutumia kisu.
Badhi walimkosoa msanii huyo kuwa kujikata sehemu zake za siri badala ya kwenda hospitalini kwa upasuaji.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment