ALIYEFANYA UKATIRI DHIDI YA MTOTO MATATANI

Polisi wamebadilisha mashtaka ya mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwa kamera akimpiga na kumtendea unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu,
kutoka kwa kosa la kutesa na sasa anakabiliwa na kosa la jaribio la mauaji.
Video hiyo iliwaudhi watu wengi sana kwenye mitandao ya kijamii ila baba yake mtoto huyo alisema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha wazazi wengine.
Mfanyakazi huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika gereza la Luzira na mahakama ya Nakawa kwa kosa la kutesa chini ya kifungo cha 41 kwenye katiba kinachoongelea dhidi ya mateso.
Mwanamke huyo sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Disemba.
Hata hivyo, msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, amesema "shtaka dhidi ya mwanamke huyo lilibadilishwa baada ya kupitiwa mwendesha mkuu wa mashitaka.
Tumuhirwe alikubali kosa la kumpiga mtoto huyo kwa kurunzi, tukio lililonaswa kwa kamera ya CCTV. Polisi walimfanyia Tumuhirwe uchunguzi wa kiakili na kubaini kuwa ana akili timamu.
Afisa mkuu wa polisi Fred Enaga, amewaonya waajiri kuchunguza mbinu zinazotumika kuwachagua wasichana wa kazi, kwa sababu matendo kama haya yanaweza kutokana na matatizo ya kisaikolojia.
Waziri wa Jinsia, Kazi na maendeleo ya jamii Bi Mary Karooro Okurut alipongeza juhudi za wazazi wa mtoto huyo Arnella "kutokana na kitendo hicho kwa mtoto. Ingekuwa mtu mwingine angemuua msichana huyo wa kazi lakini alifuata sheria. Pia tunapeleka marekebisho katika katiba kuhusu maslai ya watoto bungeni kuimarisha sheria zinazowajali watoto," alisema waziri huyo.
Polisi wamesema kuwa nia ya shambulio hilo haijatambulika na pia msichana huyo amefanyia kazi familia hiyo kwa siku 26 pekee. Wazazi wamesema kuwa mtoto huyo ametolewa hospitalini na hali yake ya afya inaimarika.
Kulingana na msemaji wa polisi Fred Enaga, kesi hiyo iliripotiwa na Baba ya mtoto Erick Kamanzi mnamo tarehe 13 Novemba katika kituo cha polisi cha Kiwatule baada ya kuona video hiyo.
Kesi hiyo ilipelekwa kwa kitengo cha polisi cha Kiira. Baada ya uchunguzi, msichana huyo wa kazi alihukumiwa na shitaka la mateso katika mahakama ya Nakawa na kuzuiliwa katika gereza la Luzira.
Bwana Enaga alisema Bi Tumuhirwe alishtakiwa chini ya kifungo cha tatu kwenye katiba kinacholinda maslahi ya watoto. Kifungo hicho kinajumuisha mashitaka kama ya kutesa inayopeana uwezekano wa kumfunga mtu hadi miaka 15 gerezani.
Hata hivyo, Bwana Enaga anashauriana na mkurugenzi wa pande za mashtaka kurekebisha hukumu hiyo kuwa kifungo cha maisha.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment