Mji wa St Louis umeshuhudia maandamano na vitendo vya uporaji baada ya jaji kupitisha uamuzi wa kumshtaki aliyemuua kijana mweusi Michael Brown.

Polisi mjini humo wamesema vurugu zimeleta madhara makubwa zaidi kuliko ya mwezi Agosti baada ya kuuawa kwa kijana huyo.
Kamanda wa Polisi wa St Louis, Jon Belmar amesema alisikia milio ya risasi takribani 150 kutoka kwenye makundi ya watu.
Brown alifyatuliwa risasi na Polisi tarehe 9 Mwezi Agosti, hali iliyoibua ghadhabu na maandamano.
Watu wengi wa jamii ya Afrika na Marekani walitoa wito wakitaka Afisa Polisi Darren Wilson ashtakiwe kwa mauaji.
Rais wa Marekani Barack Obama alitoa wito kwa wamarekani kuwa watulivu na kukubali maamuzi ya Jaji kuhusu kesi hiyo.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment