NJAMA YA POLISI KUMVUA NGUO MWANAMKE YAGONGA MWAMBA

Afisa mmoja wa polisi wa utawala nchini Kenya ni miongoni mwa wanaume waliokamatwa kwa kujaribu kumvua nguo mwanamke katika mtaa wa Komarock viungani mwa mji mkuu Nairobi.

Polisi walisema watu wanne walimzingira mwanamke huyo alipokuwa anaenda nyumbani kutoka kanisani akiwa amefuatana na rafiki yake.
Wanaume hao walijaribu kumvua nguo mmoja wa wanawake hao ila waliokolewa na wananchi waliokuwa wakielekea makwao.
Wanaume wawili waliokuwa wanawaokoa wanawake hao walijeruhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa Daily Nation, Kioo cha basi iliyokuwa barabarani pia kilivunjika katika purukushani hizo.
Polisi waliofika katika eneo la tukio waligundua kuwa mmoja wa waliowashambulia wanawake hao alikuwa afisa wa polisi.
Tukio hilo limefanyika siku chache tu baada ya mamia ya wanawake kuandamana mjini Nairobi kulaani kitendo cha kumvua mwanamke mmoja mavazi yake yakisemekana kutokuwa na heshima.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment