AYEW ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA MWAFRIKA UFARANSA




Andrew Ayew mwenye umri wa miaka 25 amewashinda Max Alain(Ivory Coast, Saint-Etienne),  na Aymen Abdennour (Tunisia, Monaco) katika tuzo za Marc-Vivian Foe na kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora mwafrika nchini Ufaransa.

Lakini pia tuzo hiyo yaweza kuwa ni tuzo ya mwisho kwake akiwa kama mchezaji Marseille kwani tayari amesema kuwa anamipango ya kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu.
Ayew amefunga magoli 10 katika mechi 27 alizocheza akiwa na miamba hiyo ya Ufaransa, mchezaji huyo amejiunga na klabu hiyo mwaka 2007 akipelekwa kwa mkopo katika klabu ya  L'Orient na Arles Avignon mwanzoni mwa usakataji kabumbu kabla ya kuwa mchezaji muhimu wa timu hiyo.
Ayew ambaye amecheza mechi 158 na kufunga magoli 43 katika timu hiyo ya Marseille anasema kuwa rais wa klabu hiyo Vicente Labrune tayari ameongelea suala hilo na hivyo kufanya jambo hilo kuwa wazi nusu nusu.
Pia aliongeza kuwa kuna vitu vingi nyuma ya maamuzi, na wanajaribu kutafuta suluhisho ambalo litapelekea yeye kubaki klabuni hapo lakini kwa pande zote mbili kumekuwa na mkanganyiko iwe ni kwa michezo ama kwa sababu za kiuchumi.
Lakini pia Ayew anasema alikuwa akitegemea zaidi na anatarajia kuona klabu hiyo ikiwa na kikosi chenye ushindani zaidi katika mwaka ujao ambapo watapigania kushinda taji la ligi na hilo halina tatizo.
Hata hivyo anasema klabu haiwezi kumpa mshahara ule ule wakati hayupo katika kiwango hicho kwa wakati huo.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa akicheza na mdogo wake Jordan kabla ya kuhamia katika klabu ya Lorient mwanzoni mwa msimu ameweza kuzivutia timu nyingi kutoka katika ligi ya Uingereza.

HAPA WACHEZAJI WALIWAHI KUCHUKUA TUZO YA MARC VIVIAN FOE
2014: Vincent Enyeama (Nigeria/Lille)

2013: Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon/Saint-Étienne)

2012: Younès Belhanda (Morocco/Montpellier Hérault SC)

2011: Gervinho (Ivory Coast/Lille)

2010: Gervinho (Ivory Coast/Lille)

2009: Marouane Chamakh (Morocco/Bordeaux)

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment