TANZANIA YAANZA KUJIFUA FAINALI ZA VIJANA AFRIKA

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) imeingia kambini jijini Dar es Salaam chini ya kocha mkuu Adolf Rishard kujiandaa na progamu ya vijana kuwania kufuzu kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar

Aidha katika kuhakikisha timu hiyo inakua tayari kwa michuano ya kuwania kufuzu kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar, timu hiyo ya vijana itafanya ziara ya mafunzo mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini kwa kucheza michezo ya kirafiki.
Mwezi Februari 2016 timu hiyo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za mikoa ya Dodoma na Mwanza, kabla ya kuelekea tena katika ziara kwenye nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya mwezi Aprili 2016.
Mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana, Ayoub Nyenzi amesema kamati yake imeandaa programu maalumu ya kuwaanda vijana kwa ajili ya kuichezea timu ya Taifa U-17 mwaka 2017.
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imeandaa program hiyo ya vijana U-15 ambao watakua kambini kwa muda siku 10, wakifanya mazoezi uwanja wa kumbukumbu ya Karume na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na timu za Azam U17 na shule ya Sekondari Makongo.
Kocha mkuu na timu yake ya U-15 atazunguka mikoa saba nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na kung'amua vipaji vingine kwa ajili ya kuboresha timu yake. Mikoa itayotembelewa ni Mbeya, Mwanza, Morogoro, Arusha, Tanga, na Dar es alaam (Ilala, Kinondoni, Temeke).
Ratiba ya CAF kuwania kufuzu kwa fainalizaAfrika 2017 inatarajiwa kuanza mwezi Juni 2016, ambapo kikosi cha Tanzania kitakua kimeshapata muda mzuri wa maandalizi kwa lengo la kuhakikisha timu inashiriki fainali hizo nchini Madagascar 2017.
 
Fainali za U-17 mwaka 2017 zinatarajiwa kufanyika nchini Madagascar, huku Tanzania ikitarajia kwa kuwa mwenyeji wa fainali hizo za vijana U-17 kwa mwaka 2019.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment