CRISTIANO RONALDO AONGOZA KWA UMAARUFU

Cristiano Ronaldo


Mchezaji nyota wa Real Madrid na Ureno Christiano Ronaldo ndiye binadamu maarufu zaidi duniani kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 amempiku Mwanamuziki maarufu kwa kunengua kiuno Shakira na wafuasi zaidi ya milioni 107.
Ronaldo anawafuasi 107,096,356 wakilinganishwa na 107,087,100 Shakira
Ronaldo aliweka rekodi kwa kuwa mchezaji maarufu zaidi duniani alipotimiza wafuasi milioni 100 mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Nyota huyo wa Real Madrid alijiunga na mtandao wa kijamii wa Facebook mwaka wa 2009.
Na si hapo alikodhibitisha udedea wake, Ronaldo ana zaidi ya wafuasi milioni 34 katika mtandao wa kijamii wa Twitter ambako anaorodheshwa katika nafasi ya 13
Msanii Katy Perry ndiye anayeongoza kwa umaarufu kwenye twitter akiwa na jumla ya wafuasi milioni 66.6.
Justin Bieber, Barack Obama, Taylor Swift, YouTube, Lady Gaga, Justin Timberlake, Rihanna, Britney Spears, Ellen DeGeneres, Instagram na Twitter ndio wanaompiku Ronaldo.
Licha ya hiyo yeye ndiye mwanaspoti maarufu zaidi kwenye mtandao huo wa Twitter.
Mshambulizi wa Brazil na Orlando City Kaka ndiye mchezaji wa pili kwa umaarufu akiwa na wafuasi milioni 22.2 million.
 
Licha ya kuwa maarufu na wafuasi wa timu ya Uingereza ya Manchester United kiungo machachari Wayne Rooney anashikilia nafasi ya 95 katika mtandao huo akiwa na wafuasi milioni 10.8 million.
Katika Facebook hata hivyo, Mchezaji bora mara nne duniani na Mshambulizi wa Barcelona ,Lionel Messi ndiye mwanaspoti wa pili kwa umaarufu duniani.
Messi anawafuasi milioni 78.

Nyota wa zamani wa England David Beckham anafunga orodha ya tatu bora kwa wafuasi milioni 52
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment