WABUNGE WATAKA WANAFUNZI WAFUNDISHWE SOMO LA NGONO

 

Shule zote za serikali zikiwemo za msingi na zile za upili nchini Uingereza zitalazimika kufunza somo la ngono na uhusiano SRE ,wabunge wa taifa hilo wamesema katika ripoti yao,,

Kamati ya elimu katika bunge la Uingereza ilianzisha uchunguzi baada ya kubainika kuwa zaidi ya theluthi moja ya shule zilikuwa zikishindwa kutoa mafunzo ya somo hilo kwa umri unaohitajika.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Graham Sturat amesema kuwa vijana wadogo wana haki ya kupata habari ambazo zitahakikisha usalama wao.
Serikali imesema kuwa itaangazia matokeo ya ripoti hiyo.
Mwaka 2013 ripoti ya bunge hilo ilisema kuwa masomo ya kibinafsi,ya kijamii ,afya na elimu ya kiuchumi ambapo somo hilo la ngono limehusishwa yanahitaji kuimarika katika asilimia 40 ya shule.
 
Wabunge hao wamesema:Hali hii haitakubalika katika masomo mengine licha ya kuwa harakati za serikali kuimarisha masomo hayo ni za kiwango cha chini.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment