Barrack Obama |
Kauli ya Rais Barack Obama ya kuwataka Wakristo kujua kuwa Uislamu si dini pekee inayohusishwa na vurugu na mauaji, imezua kizaazaa duniani na baadhi wameanza kuhoji kama kiongozi huyo wa kwanza mweusi wa Marekani ni Mkristo..
Obama alitoa kauli hiyo Jumatano wakati wa Siku ya
Taifa ya Maombi (National Breakfast Prayer) alipofananisha Vita vya
Msalaba na vitendo vya ugaidi vinavyofanywa na vikundi vya Kiislamu
vyenye imani kali.
“Hadi tutakapokuwa juu ya farasi na kufikiri kuwa
jambo hili ni la pekee kwa baadhi ya sehemu, kumbuka kwamba wakati wa
Vita Vitakatifu (crusades) na Mahakama ya Kanisa Katoliki (Inquisition),
watu walifanya vitendo vya kutisha kwa Jina la Kristo,” Obama
alikaririwa na Shirika la Habari la AFP akizungumza kwenye hafla hiyo
Jumatano.
“Na katika nchi yetu, utumwa na sheria za kibaguzi (Jim Crow), zote pia zilihalalishwa kwa jina la Kristo.”
Obama alikuwa akitoa hotuba yake kuhusu dini
kwenye hafla hiyo iliyofanyika Washington, D.C. Akitumia maandiko ya
dini za Kiislamu, Kiyahudi na kikristo, Obama alisifu imani yake.
“Utamaduni wa maombi umetuweka pamoja, ukitupa
nafasi ya kukusanyika kwa unyeyekevu mbele ya Mungu na kutukumbusha nini
kinatakiwa kushirikiana kama watoto wa Mungu,” alisema.
Obama pia aliwageukia magaidi wa kijihadi aliosema
“wanaasi Uislamu”. Alilinyooshea kidole kundi la Islamic State ambalo
alisema “limefanya vitendo visivyoweza kutamkwa vya ukatili “ Mashariki
ya Kati pamoja na wanamgambo ambao hivi karibuni waliua watu kadhaa
kwenye ofisi za gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo nchini Ufaransa.
Lakini kauli yake imekosolewa sehemu mbalimbali.
Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki
Tanzania (TEC), Padri Saba Raymond alisema alichozungumzia Obama ni
historia na hivyo dunia inatakiwa ijifunze.
“Kama kimetokea, kimetokea. Tunatakiwa kujifunza
kutokana na kilichotokea. Katika ulimwengu wa sasa ni fursa ya kujifunza
yale yaliyotokea na hayafai na wakati huu yasitokee tena... wale
wanaoyataka, washindwe,” alisema Padri Raymond
Padri Raymond aliongeza kusema: “Utumwa ulikuwa
haufai na Marekani walijihusisha kwa hili (kuuondoa) na hii ni historia
ambayo wanapaswa kuiacha.”
Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho
alisema:” Ni kauli ya kujihami na anaogopa kuwanyooshea kidole moja kwa
moja... Wamarekani wasingependa yatokee kama yaliyowahi kutokea huko
nyuma.
Credit; BBC
Credit; BBC
0 comments :
Post a Comment