DULLY SYKES AONDOKEWA NA BABA YAKE MZAZI

Abby Sykes ambaye ni baba wa mwanamuziki Dully Sykes enzi ya uhai wake.

Mzee Abby Sykes ambaye ni Baba mzazi wa muimbaji wa muziki wa Bongo Fleva Prince Dullysykes,amefariki saa 8 mchana wa leo akiwa hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa ameenda kwaajili ya kupatiwa matibabu,,

Dully sykes ameelezea kitu kilichosababisha umauti wa Mzee Abby sykes na kusema ''Mzee alikua ana vidonda katika miguu ndiyo chanzo kikubwa,sumu ikasambaa ikasababisha kifo chake,vidonda vilishindwa kupona kwa ajili ya moshi wa sigara,hakua na tatizo lolote''
Pia Dully aliongeza kuwa ''Mzee vidonda alianza kuugua kwa miezi 4,miezi 2 alikua anavumilia tu lakini miezi 2 ya mwishoni ndiyo ilizidi kumsumbua,mazishi tunategemea kuyafanya kesho saa 10 kwenye makaburi ya Kisutu,lakini safari ya kwenda msikitini tutaanza saa 7 mchana.''
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment