Ronaldo luis nazario de lima mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil. |
HAKUNA kisichowezekana katika soka. Miguu bado inamuwasha Ronaldo de Lima na amedai kwamba anafikiria kurudi tena uwanjani kukipiga katika timu anayoimiliki, Fort Lauderdale Strikers, inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Marekani.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi Jumatano,
ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu awe mmoja wa wamiliki wa klabu hiyo,
Ronaldo alisema kwamba anataka kurudi uwanjani kuisaidia timu hiyo.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 38 aliyeiwezesha
Brazil kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2002, hajacheza soka tangu mwaka 2011
wakati alipoachana na klabu ya kwao Brazil, Corinthians.
Amedai kwamba anataka kurudi uwanjani akiwa mchezaji wa akiba ingawa amekiri kwamba mchakato mzima utakuwa mgumu.
“Napenda kucheza, napenda soka, soka lilikuwa
maisha yangu. Ni mapenzi yangu makubwa. Nilipostaafu niliacha kwa sababu
ya mwili wangu. Nilikuwa nasikia maumivu makali na nilikuwa majeruhi,”
alisema Ronaldo.
“Hata hivyo kucheza soka inabidi uwe katika hali
nzuri. Nitajaribu kufanya hivyo. Ni changamoto nyingine. Nina uhakika
nitaisaidia ligi na nitaisaidia timu pia. Nitafanya sana mazoezi na kama
kocha atanihitaji basi hauwezi kujua.
Ronaldo akishangilia enzi hizo katika timu yake ya taifa ya Brazil. |
“Nitajaribu kucheza baadhi ya mechi. Mwaka huu
nataka nifanye sana mazoezi. Miaka mitatu iliyopita sikufanya hivyo kwa
sababu nilikuwa bize na mambo mengine. Labda kama tutafika fainali na
nitakuwa najisikia vizuri kwanini nisicheze? Nitaweka jina langu katika
orodha ya timu nikiwa mchezaji wa akiba.
“Nimefanya mambo mengi tofauti miaka ya karibuni.
Mwaka jana nilikuwa katika Kombe la Dunia nikiwa mmoja kati ya
waandaaji, pia nilikuwa nachambua mechi za michuano hiyo katika kituo
cha TV cha Globo.
“Na sasa nimepata nafasi nzuri ya kuongoza timu
nikiwa mmiliki. Fort Lauderdale Strikers ni timu yenye historia na
utamaduni. Marekani soka linakuwa kwa hiyo nadhani ni nafasi nzuri
sana.”
Ronaldo |
Ronaldo anakumbukwa kwa kufanya mambo makubwa
barani Ulaya akizichezea klabu za PSV Eindhoven, Barcelona, Inter na
Real Madrid. Anakumbukwa pia kwa kufunga mabao mawili murua dhidi ya
kipa wa Ujerumani, Oliver Kahn, katika pambano la fainali ya Kombe la
Dunia mwaka 2002 nchini Japan.
0 comments :
Post a Comment