KINGUNGE; KATIBA MBOVU INADUMAZA MAENDELEO

Mzee Kingunge Ngombare Mwiru ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania.

Uchumi wa Tanzania utaendelea kudumaa kama itaendelea kung’ang’ania Katiba isiyokuwa na misingi bora ya maendeleo ya uchumi...
Hayo yalisemwa na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru mjini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kwa kushirikiana na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) .
Wakati kiongozi huyo akisema hayo, mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed amesema kama siyo Muungano, Zanzibar ingekuwa imeshapinduliwa zaidi ya mara 10.
Kingunge, aliyekuwa mjumbe wa Bunge la Katiba, alisema licha ya Tanzania kuonekana inapiga hatua, asilimia kubwa ya uchumi wake bado ni tegemezi hivyo inahitaji kuwa na katiba bora itakayoweka misingi ya maendeleo ya uchumi .
 “Tatizo hili liko katika nchi nyingi za Afrika na hasa za Waafrika weusi, uchumi wake bado ni tegemezi,” alisema Kingunge.
Alisema historia inaonyesha Waafrika pamoja na kujikomboa kutoka katika mikono ya wakoloni, bado ni wanyonge kwa sababu ya kushindwa kujijengea uchumi imara usiotegemea nchi nyingine.
Alisema kama Waafrika wataendelea kuridhika na mwendo wa kutumia vitu vinavyotengenezwa na nchi nyingine, ipo siku ukoloni utarejea katika nchi hizo.




Credit; Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment