PICHA ZA MTOTO ZAPELEKEA BABA KUJITOA UHAI

Loredana Chivu mwanamitindo kutoka nchini Romania.

Baba mmoja amejiua baada ya kuona picha za uchi za mwanawe wa kike katika jarida la Playboy nchini Romania..

Loredana Chivu alirarua ukurasa uliokuwa na picha yake akiwa 'amepoz' katika jarida hilo la Playboy na punde baba yake alipogundua kuhusu picha hizo, alizongwa na mawazo na hata kumkana mwanawe.
Kwa mujibu wa mtandao wa Mirror, msichana huyo mwenye umbo la kuvutia alisema, '' baba yangu aliacha kuongea na mimi na kuonekana mwenye hasira sana''.
"alipogundua kuwa picha hizo zilikua zangu, alijitenga sana na kujaribu kunitenga na mimi''.
Nilidhani labda angesahau na sikudhani hata siku moja angejitoa uhai.
 

Mwanamitindo huyo Loredana Chivu mwenye mamia ya picha akiwa nusu uchi kwenye akaunti yake ya Instagram, alikuwa na uhusiano wa karibu sana na babake lakini alisema yote hayo yalibadilika baada ya bab a yake kuona picha zake akiwa nusu uchi.
Alipokwenda kumtembelea baba yake miezi michache baadaye, baada ya kuamua kwamba kimya kilikuwa kimeendelea kwa muda mrefu sana, alishtuka sana kumpata baba yake akiwa amejitoa uhai
"nilimpata akiwa na kamba shingoni akiwa ananing'inia chumbani''.
Loredana,anayeishi nchini Romania, anasema kuwa tangu kifo cha baba yake, amekuwa akiwaza na kuwazua kwamba aliamua kujiua kwa sababu ya mgogoro kati yetu na hasa kuhusu picha zangu alizoziona kwenye jarida la Playboy.
''Najuta sana kwamba sikuwahi kupata muda wa kuzungumza na baba yangu kuhusu yaliyotokea''.
''Hakuacha ujumbe wowote kabla ya kujitoa uhai, siku zote tulikuwa na uhusiano mzuri lakini yote yalibadilika baada ya baba kuona picha zangu nikiwa uchi. Bado inaniuma sana na nisingemtakia mtu yeyote kupatwa na kama yaliyonikuta''.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment