MTOTO WA MIAKA 8 AHOJIWA KUHUSU UGAIDI

Mtoto mwenye umri wa miaka 8 alihojiwa na polisi nchini Ufaransa kwa nusu saa Jumatano baada ya madai kwamba alitoa matamshi ya kuwasifu magaidi akiwa shuleni.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la AP, mtoto huyo alikataa kuungana na wenzake darasani kwa kimya cha dakika moja kuwakumbuka watu 12 waliouawa na wanaume wawili waliokuwa wamejihami mjini Paris Ufaransa mapema mwezi huu.
Shambulizi lilitokea katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo Januari tarehe saba kufuatia hatua ya jarida hilo kuchapisha picha za kumkejeli mtume Mohammad wa dini ya kiisilamu.
Wahariri wakuu wa jarida hilo pamoja na wafanyakazi wenginge waliuawa.
Mwalimu wa mtoto huyo alisema kuwa hakukataa tu kuungana na wenzake kwa kimya cha dakika moja bali pia aliwasifu washambuluaji.
Na kwa sababu ya hali ya usalama ilivyo nchini Ufaransa kwa sasa, mwalimu mkuu aliamua kumripoti mtoto huyo kwa polisi. Hata hivyo afisa mmoja alisisitiza kwamba hakuna malalamiko yaliwasilishwa dhidi ya mtoto huyo.
"tulimwita mtoto huyo na babake kujaribu kuelewa ni vipi mtoto mwenye umri wa miaka 8 ana mawazo ya itikadi kali hivyo,'' alisema Marcel Authier afisa mkuu wa mawasiliano katika eneo hilo.
"bila shaka mtoto huyu haelewi anachosema lakini ni muhimu kwetu kuhoji mawazo kama haya'' alisema Marcel.
Wakili wa mtoto huyo, Sefen Guez Guez, hakuweza kupatikana kwa maoni yake lakini kwenye akauti yake ya Twitter alisema kuwa mtoto huyo alikiri kusema: ''Ninawaunga mkono magaidi''.
Wakati polisi walipomhoji maana ya ''ugaidi'' mtoto huyo alisema '' sijui''
" Baba huyo na mtoto wake walishangazwa na namna walivyohojiwa, hali inayoonyesha wazi wasiwasi ambao umeikumba Ufaransa tangu mashambulizi yaliyofanywa mapema mwezi huu'' ilisema taarifa ya shirika linalopambana na hofu dhidi ya waisilamu.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment