MCHEZAJI AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI



Gasan Magomedov aliyefariki baada ya kupigwa risasi.


Gasan Magomedov mwenye umri wa miaka 20 anayeichezea klabu ya Urusi Anzi Makhachkala ameuawa kwa kupigwa risasi karibu na nyumbani kwake kazkazini mwa Caucusus nchini Urusi.

Mogomedov alikuwa akiendesha gari lake wakati wa mfyatuliano wa risasi ndipo gari lake likamiminiwa risasi na kumpelekea kuaga dunia kutokana na majeraha aliyopata wakati alipokuwa akisafirishwa kuelekea hospitali.
Gasan Magomedov mbele enzi ya uhai wake akiwa na wachezaji wenzake wa klabu ya Anzi Makhachkala.

Kulingana na kilabu hiyo ya Anzhi hakuna mtu aliyekamatwa na sababu ya tukio hilo haijulikani.
Klabu hiyo imetuma rambirambi zake kwa familia ya Magomedov,mchezaji wa kiungo cha kati.
Hakuna ripoti za majereha mengine kufuatia kisa hicho.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment