Rais wa Serikali ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein. |
Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar imepitisha azimio la pamoja la kumtaka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kujitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais uchaguzi unaotarajia kufanyika mwaka huu,imefahamika Visiwani humo.
Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa
akiwasilisha mada kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
katika Kongamano lililofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Fidel
Castro na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, huko
Pemba.
Alisema kwamba maamuzi hayo yamelazimika kufanyika
baada ya kufanyika tathimini na kuona Dk Shein ameonyesha mwelekeo
mzuri wa kisiasa na kiuchumi katika kipindi cha uongozi wake kutokana na
utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi baada ya kushika wadhifa huo
mwaka 2010.
“Kamati maalum ya Halmashauri Kuu Zanzibar
tumepitisha makubaliano na kumuomba aongeze kipindi kingine cha kugombea
Urais kwa sababu ametekeleza vizuri ilani ya uchaguzi, sasa imebakia
hiyari yake.”alisema Aboud ambaye Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya
Chama hicho.
Aidha alisema kwamba katika kipindi chake Dk Shein
ameonyesha uwezo, busara na hekima kubwa katika kuiongoza Serikali ya
Umoja wa Kitaifa (SUK) na kufikia malengo ya kuanzishwa kwake ikiwemo
kuondoa siasa za chuki na kujenga misingi ya umoja wa kitaifa kwa
wananchi wake.
“Wakati ukifika tumekubaliana katika Kamati
Maalum Dk Shein achukuwe fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa
Zanzibar.”alisema Aboud na kuibua shangwe kwa washiriki wa Kongamano
hilo.
Mwaka 2005 Makamu wa Rais Muungano Dk Mohamed
Bilal alijitokeza kuchukua fomu na kuchuana na Rais mstaafu Amani Abeid
Karume na kuibua hekaheka kubwa ya kisiasa kabla ya kuombwa kuondoa jina
lake na wazee kwa madhumuni ya kulinda umoja katika kuelekea Uchaguzi
Mkuu.
Credit; Mwananchi
Credit; Mwananchi
0 comments :
Post a Comment