ASILIMIA MOJA YA WATU MATAJIRI DUNIANI

Matajiri wakubwa Duniani Bill Gates(kulia) akiwa na Warrren Buffett.


Huku wafanyibiashara na wanasiasa wa ngazi za juu wakikutana katika mkutano wa kiuchumi duniani mjini Davos wiki hii ,hisia tofauti zimetolewa kuhusiana na kuwepo kwa ukosefu wa usawa duniani bila kuisahau asilimia moja ya watu Matajiri duniani.

Matajiri hao wanaishi katika visiwa vya kibinafsi,lakini je, hao ndio matajiri wanaojulikana Pekee?.
Ripoti moja ya shirika la wahisani la Oxfam iliotolewa sanjari na mkutano huo wa Davos,ilizua hisia kali baada ya kubashiri kwamba asilimia moja ya matajiri duniani huenda ikamiliki idadi yote ya watu duniani.
Ilitoa utafiti wake kutoka kwa benki ya Credit nchini Uswizi ambayo inakadiria jumla ya utajiri katika kila nyumba kuwa dola trillioni 263.
Huo ni itajiri na wala si mapato.
Watu matajiri kama vile Bill gates ,Warren Buffett na Mark Zuckerberg ni miongoni mwa asilimia 1.
Mack Zuckerberg

Lakini je, ni nani mwingine aliyeorodheshwa katika asilimia hiyo?.
Kulingana na ripoti hiyo ya benki ya Credit watu wengine millioni 47 wana utajiri wa dola 798,000 kila mmoja.
Hiyo inashirikisha watu wengi katika mataifa tajiri ambao pengine wasingejitambulisha kama matajiri,lakini ambao wanamiliki nyumba ama wamelipa kiwango kikubwa cha mkopo.
Miongoni mwao ni:
Watu millioini 18 wanatoka Marekani
Millioni 4 inatoka Japan
Watu millioni 3.5 wanatoka Ufaransa
Watu millioni 2.9 wanatoka Uingereza
Millioni 2.8 wanatoka Ujerumani
Millioni 4 inatoka Japan
Na millioni 1.6 inatoka China.





Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment