AFCON; AYEW AIPELEKA GHANA ROBO FAINALI

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ghana Andre Ayew.

Andre Ayew alifunga goli katika dakika za mwisho za mpambano kati ya timu yake ya Ghana na Afrika Kusini, ukiwa ni mchezo wa kundi C wa kufuzu kucheza robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zinazofanyika nchini Equatorial Guinea.
Ayew kwa ushujaa alipiga mpira wa kichwa golini mwa Afrika Kusini kufuatia krosi iliyopigwa kutoka upande wa kushoto na Baba Rahman.
Kabla ya goli hilo ilionekana kama Ghana imetolewa katika michuano hiyo.
Katika mchezo huo, Afrika Kusini ilikuwa inaongoza kwa bao la Mandla Masango, ambalo huenda ni bao la mashindano ambalo lilifungwa umbali wa yadi 25.
Ghana ilizidisha mashambulizi baada ya mapumziko na mchezaji wa akiba John Boye alisawazisha goli kabla ya Ayew kupigilia msumari wa mwisho.
Zikiwa zimebaki dakika 17, Ghana walikuwa wanaelekea kurudi nyumba kwani walikuwa nyuma kwa goli 1-0 lakini goli la Boye, liliwapa matumaini na ndipo Ayew alipowahakikishia Ghana kuongoza kundi C mbele ya Algeria ambayo nayo iliishindilia Senegal magoli 2-0.
Jumatano ni michezo ya kundi D yenye timu za Cameroon, Ivory Coast, Guinea na Mali. Kundi hili ndilo tata zaidi kwani timu zote zinafanana kwa kila kitu zikiwa na pointi mbili kila moja na idadi sawa ya magoli ya kufunga na kufungwa. Hivyo kila timu ina nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali.
Katika michezo hiyo, Cameroon inavaana na Ivory Coast, huku Guinea ikipambana na Mali.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment