MWANAFUNZI ALIYEKUA AKINADI UBIKRA AKOMA

Mwanafunzi anayesomea udaktari nchini Marekani ambaye alikuwa ana nadi ubikra wake, amesitisha shughuli hiyo baada ya watu wachache sana kujitokeza wakiwa tayari kuulipia ubikra wa mwanamke huyo.

Pamoja na hilo Kern hakua na uhakika kuhusu ukweli wa waliojitokeza kulipia ubikra wake.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Daily Mail.
Mwanafunzi huyo, Hanna Kern alikuwa ananadi ubikra wake chini ya jina ambalo sio lake 'Elizabeth Raine'.
Kern ana umri wa miaka 28 na ana digrii ya uzamifu katika chuo kikuu cha Washington, nchini Marekani.
Jarida lingine la Huffington Post, amejitambulisha kwa jina analojulikana nalo.
Kern anakuwa mwanafunzi wa hivi karibuni aliyenadi ubikra wake kwenye mtandao ambao amelazimika kuusitisha baada ya kukosa kupata kima alichokitaka na hata pia kukosa kupata wanaume wengi waliovutiwa na kampeini yake na kuhofia kuwa waliojitokeza sio watu wakweli.
Alikuliwa akisema baada ya kukosa kufanikiwa, amepata funzo na kujua kwa nini kampeni kama hizi huwa hazifanikiwi.
Wa mwisho aliyejitokeza kulipia ubikra wake alikuwa ametoa kima cha dola 801,000,lakini mwanafunzi huyo aliamua kutoendelea na juhudi zake kwani hakufurahishwa na pesa hizo.
''Nimeamua kusitisha kampeni yangu, na kurejea katika msomo yangu ya udaktari.''
''Bado ninaamini kuwa ubikra ni kitu kizuri na pia ninaamini kuwa mwanamke anapaswa kuachwa afanye anavyotaka, '' ingawa kwa sasa masomo ndio ninayotaka kushughulika nayo kwa sasa,'' alisema Kern.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment