MSHINDI WA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA,BBC

Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika BBC mwaka huu amepatikana.Baada ya maelfu ya kura kuhesabiwa, mchezaji wa Algeria na nyota wa Porto,
Yacine Brahimi ndiye mshindi wa mwaka huu.
Hapajawahi kutokea katika miaka 23 ya historia ya shindano hilo kwa mchezaji bora kutoka Algeria kuishinda, lakini Brahimi amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya mwaka uliokuwa na mbwembwe wa 2014.
Aliingiza bao la ushindi dhidi ya mabingwa wa Hispania Barcelona, bao lingine la kisasa katika ligi ya mabingwa wa ulaya na kisha kuwa katika msitari wa mbele wakati nchi yake iliposonga mbele katika michuano ya kombe la dunia.
Hiyo ilikuwa historia kwa Algeria kufika katika awamu ya muondoano katika dimba hilo.
Hii bila shaka ilikuwa nafasi nzuri kwa mashabiki wa BBC pamoja na wapenzi wa soka kumchagua kama mchezaji bora zaidi wa Afrika mwaka huu.
Aliwapiku wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast na hatimaye Yaya Toure - aliyenyakua ushindi mwaka jana.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment