MISAADA INAHITAJIKA ZAIDI MWAKANI

Mkuu wa kitengo cha misaada cha Umoja wa Mataifa Valerie Amos ,amesema kwamba hali ya sasa nchini Syria ni doa katika jamii ya kimataifa
,ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mkakati mkubwa wa misaada ya kibinadamu kuwahi kutokea.
Bi Valie Amos amesema kwamba zaidi ya dola milioni kumi na sita zinahitajika kusaidia harakati za Umoja wa mataifa duniani kwa mwaka ujao,na nusu ya fedha hiyo inahitajika nchini Syria pekee.
Umoja huo umesema kwamba wa Syria wapatao milioni tatu wameikimbia nchi yao kufuatia mapigano yanayoendelea na kukimbilia nchi jirani na wengine milioni kumi na mbili wenye uhitaji wakiwa wametawanyika nchini humo.
Juma lililopita kitengo cha chakula cha umoja huo,kililazimika kupunguza kiwango cha misaada ya chakula kwa wakimbizi wa Syria kutokana na ukosefu wa misaada ya kibinadamu.
Inaarifiwa kwamba kiasi cha dola za kimarekani bilioni kumi na tatu kilichoombwa na umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2014 hawakupewa zote.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment