MANCHESTER UNITED YAICHAPA LIVERPOOL

Kilabu ya Manchester United imeicharaza Liverpool mabao matatu bila jibu katika mechi ya kasi iliojaa mashambulizi makali kutoka pande zote mbili.

Hatahivyo ni Manchester United walioona lango la Liverpool kupitia bao la nahodha wao Wayne Rooney katika kipindi cha kwanza.
Yuan Mata alifanya matokeo kuwa mbili bila baada ya kufunga kwa krosi iliyopigwa na Young,bao ambalo wachezaji wa Liverpool walidhani ni la kuotea.
lakini Licha ya Liverpool kunoa safu yao ya mashambulizi na kuvamia ngome ya Manchester United kupitia Sterling aliyekosa mabao ya wazi Manchester united iliendelea kufanya mashambulizi kupitia Van Persie na Rooney.
Liverpool ilimuingiza Mario Balotelli ambaye pia naye alikosa mabao ya wazi huku Kipa wa Manchester akinyaka mashambulizi hayo.
Na baada ya dakika kadhaa Robin Van Persie alifanya mambo kuwa 3-0 baada ya safu ya ulinzi ya Liverpool kufanya masihara katika lango lao.
Pongezi nyingi zinaenda kwa golikipa wa Manchester United David De Gea kwa kuokoa michomo mingi ya washambuliaji wa Liverpool  isiingie langoni mwake na hivyo kuibuka kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo .
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment