DUNIA YATAKIWA KUTOISAHAU SUDAN KUSINI

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, ICRC, limeonya kuwa mwaka mmoja baada ya ghasia kuzuka Sudan Kusini
mapambano bado yanaendelea baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji na kuhatarisha raia.
Mkuu wa ICRC nchini humo, Franz Rauchenstein, alisema ingawa waandishi wa habari wameipa mgongo Sudan Kusini, wale walionasa katika vita hivyo haifai kuwasahau.
Mapigano yalizuka Disemba mwaka jana baina ya wanajeshi wa Rais Salva Kiir na wale watiifu kwa makamo wake wa rais wa zamani, Riek Machar.
Watu kama milioni moja na nusu wamepoteza makaazi na mashirika ya misaada yanasema msaada wa kimataifa unahitajika kuepusha upungufu mkubwa wa chakula.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment