LIONEL MESSI KUPEWA TUZO YA HESHIMA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi.


Chama cha soka cha Hispania (LFP) kimetangaza kutoa tuzo kwa Lionel Messi ambapo ni tuzo ya heshima kwa kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa la liga kwa muda wote.

Messi amevunja Rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Telmo Zarra ya kufunga Bao 251 alipofunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Sevilla.
Rais wa chama cha soka cha Hispania Javier Tebas, amethibitisha kuwa watatoa tuzo hiyo kwa mshambuliaji huyo wa timu ya Barcelona.
Messi atapewa Tuzo hiyo Januari 11 katika Uwanjani Nou Camp wakati Barca itakapocheza Mechi dhidi ya Atletico Madrid.
Mpaka sasa Messi, amekwisha funga jumla ya mabao 258 katika ligi ya Hispania, huku hasimu wake wa karibu Cristiano Ronaldo akiwa nafasi ya tisa katika historia ya ufungaji bora wa muda wote.



Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment