WATU 7000 WAPOTEZA MAISHA KWA EBOLA

Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO, zinaonesha kuwa watu karibu 7,000 wamefariki hadi sasa kutokana na Ebola,
karibu wote Afrika Magharibi.
Hao ni watu zaidi ya elfu moja kuliko idadi iliyotangazwa na WHO Jumatano tu.
Vifo vingi zaidi vimesajiliwa Liberia.
WHO inasema watu zaidi ya 16,000 wameugua Ebola hadi sasa.
Waandishi wa habari wanasema kuongezeka kwa idadi ya waliokufa siyo lazima inamaanisha ugonjwa unazidi kutapakaa kwa kasi kwa sababu takwimu nyengine ni za zamani.
Na Rais Francois Hollande wa Ufaransa amezuru Guinea, kiongozi wa kwanza asiyekuwa Muafrika kuzuru moja kati ya nchi tatu za Afrika Magharibi zilizoathirika sana na Ebola.
Bwana Hollande alisema alitaka kuleta ujumbe wa matumaini kwa watu wa Guinea:
"Ufaransa inaweka mfano - tumefanya hivyo kifedha kwa kutoa dola 125 milioni.
Lakini mbali ya msaada wa mali, utu ndio muhimu zaidi.
Na Guinea inapochukua hatua za kuuguza na kuzuwia Ebola isisambae, hivyo inasaidia ulimwengu, Ulaya pamoja na Ufaransa zisije nazo zikapata virusi hivyo vibaya.
Kwa hivyo tuko nanyi katika mapambano haya, vita hivi.
Na ni muhimu kuwa miaka 15 baada ya rais wa mwisho wa Ufaransa kuzuru Guinea, kuwa nami niko hapa kuonesha urafiki, umoja na matumaini."
Rais Alpha Conde wa Guinea alisema Rais Hollande amefika wakati mzuri ili kuonesha kuwa mtu yoyote anaweza kuzuru Guinea.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment