OPERESHENI MPYA YA WAKURDI DHIDI YA DOLA LA KIISLAMU

Wakisaidiwa na mabomu yakutokea angani ya Marekani wapiganaji wa Kikurdi wa Peshmerga wameyashambulia maeneo yaliyodhibitiwa na kundi la Dola la Kiislamu wakati wa msimu wa kiangazi mwaka huu.
Harakati hiyo iliyalenga maeneo katika mikoa ya Diyala na Kirkuk. Maeneo hayo yametekwa na kundi hilo wakati wa operesheni iliyofanywa mnamo mwezi Agosti ambapo kundi la Dola la Kiislamu liliidhibiti theluthi moja ya Iraq.
Kama sehemu ya mashambulizi hayo wapiganaji wa Peshmerga wakishirikiana na vikosi vya Iraq waliikomboa miji ya Sadiya na Jalula mkoani Diyala. Katika mkoa wa Kirkuk, Wakurdi wakisaidiwa na muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya Dola la Kiislamu walilenga kulikomboa eneo karibu na mji wa Karbaroot, kiasi kilometa 35 magharibi mwa mji wa Kirkuk.
Mashambulizi hayo mapya yanakuja huku waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akikamilisha vipengee vya mwisho vya mpango utakaoiwezesha nchi yake kutoa mafunzo kwa waasi kupambana na wapiganaji wa Dola la Kiislamu nchini Syria. Uturuki imekuwa ikitia na kutoa kuwasaidia wakurdi wanaopigana na kundi hilo katika mji uliozingirwa wa Kobane kwa hofu ya kuimarisha azma ya Wakurdi ya kutaka taifa lao huru nchini humo. Erodgan ameikataa miito inayoitaka Uturuki ichukue jukumu
kubwa zaidi katika mapambano dhidi ya Dola.





Credit; DW
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment