Hofu ya Ebola nchini Mali ilianza na muuguzi mgonjwa katika hospitali inayowatibu matajiri na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa mjini Bamako
aliyegunduliwa kuwa na ugonjwa huo baada ya kufa. Muda mfupi baadaye madaktari walianza kumchunguza mzee wa umri wa miaka 70 aliyekufa kutokana na Ebola baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo kutokea Guinea akiwa na matatizo ya figo. Mpaka sasa watu watatu wamekufa kutokana Ebola nchini Mali huku vifo vingine viwili vikishukiwa katika mji mkuu Bamako.
Mjumbe mkuu wa shirika la afya duniani WHO nchini Mali, Ibrahima Fall, ameonya kuhusu visa vipya vya maambukizi ya Ebola nchini humo. "Tunahitaji kuiangalia hali halisi. Kama tunawafuatilia watu zaidi ya 200, tunahitaji kugundua kwa haraka kisa kipya cha maambukizi. Hili linaweza kutokea na tunahitaji kujiandaa. Timu ziko nyanjani kuwafuatilia mara mbili kwa siku, tukitarajia kugundua visa vipya. Inawezakana."
Marekani imetangaza jana itawachunguza abiria wote wanaowasili kutokea Mali. Mali inajiunga na Sierra Leone, Guinea na Liberia kama nchi ambazo wasafiri wake wanalazimika kuchunguzwa kama wana Ebola pindi wanapowasili Marekani. Uchunguzi huo unaanza leo kwa wasafiri 15 hadi 20 wanaowasili kila siku kutoka Mali. Uamuzi huo umechukuliwa huku daktari wa Marekani, Martin Salia, akitibiwa Ebola katika hospitali ya Nebraska huko Omaha, akiwa katika hali mbaya sana tangu alipowasiri kutoka Sierra Leone.



Credit; DW
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment