GARI INAYOTUMIA KINYESI YAZINDULIWA

Basi la kwanza nchini Uingereza linalotumia kinyesi na uchafu unaotokana na chakula limeanza safari yake ya kwanza.

Bio Bus,lenye viti 40 na ambalo linatoa huduma ya uchukuzi kati ya Bath na uwanja wa ndege wa Bristol ,linaweza kusafiri hadi maili 186 kwa kutumia tangi moja la gesi.
Gesi hiyo hupatikana kupitia kutibu maji taka na uchafu wa chakula usiofaa kwa matumizi ya binaadamu.
Uchafu unaopatikana katika abiria wa basi moja unaweza kutumiwa kutoa kawi ya kulisafarisha basi hilo kutoka Lands End hadi John O'Groats.
Basi hilo ambalo limepewa majina kadhaa ya kutungwa likiwemo lile la Basi la pili linapongezwa kama njia mojawapo ya kuchochea usafiri wa umma huku ukiimarisha ubora wa hewa jijini.
Gasi inayotumiwa kuliendesha gari hilo hutoka katika mradi wa maji taka wa Bristol ambao husimamiwa na GENeco ambayo ni kampuni tanzu ya Wassex Water.
Mohammed saddiq,meneja mkurugenzi wa kampuni ya GENeco ,anaamini chakula na maji taka yanaweza kutoa kawi ya Biomethane inayotoa gesi katika shirika la kitaifa la gesi inayoweza kutoa gesi yenye uwezo wa kutumika katika nyumba 8,500 mbali na kuliendesha basi hilo la Bio.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment