RAIA 115 WA AFRIKA KUSINI WAFARIKI NIGERIA


Muhubiri T.B Joshua amewashangaza wengi kwa kusema aliona ndege ikizunguka jengo hilo kabla ya kuporomoka


Serikali ya nchini Afrika Kusini inasema kuwa watu miamoja na kumi na tano(115) wengi wao wakiwa raia wa Afrika Kusini, walifariki dunia baada ya kanisa kuporomoka nchini Nigeria.
Idadi kamili ya raia wa Afrika Kusini waliofariki ilikuwa 84.

Ndege iliyowabeba manusura wa mkasa huo, kumi na sita (16) kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya, imewasili mjini Pretoria.
Lakini pia zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea kanisa hilo la "All Nations" mjini Lagos, ambalo linaongozwa na mhubiri T.B. Joshua.
Inaarifiwa kuwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.
Mhubiri TB Joshua, amezua wasiwasi baada ya kuzungumzia juu ya kuona ndege iliyokuwa inazunguka juu ya kanisa hilo kabla ya jengo lenyewe kuporomoka.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment